1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Chissano ashinda tuzo ya Mo Ibrahim

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Da

Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano ameshinda tuzo ya kwanza ya Mo Ibrahim ambayo hutunukiwa kiongozi wa mataifa ya Afrika kutoka na uongozi mzuri uliotia fora.

Chissano ambaye anapongezwa kwa kuleta amani nchini Msumbiji amekuwa akiwekewa matumaini makubwa ya kunyakuwa tuzo hiyo.Tuzo hiyo iliotangazwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ina thamani ya dola milioni tano.

Tajiri wa simu za mkono Mo Ibrahim anadhamini mradi wa tuzo hiyo kwa matumaini ya kusaidia kuboresha utawala bora barani Afrika.

Chissano ameitowa Msumbiji kwenye dimbwi la umwagaji damu la vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuingiza kwenye amani na maendeleo wakati wa uongozi wake wa miaka 19.