1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Malaysia

Malaysia ni nchi ya kusini-mashariki mwa Asia inayokalia sehemu ya rasi ya Malay na kisiwa cha Borneo. Inafahamika kwa fukwe zake, misitu ya mvua, mchanganyiko wa tamduni za Maey, China, Uingereza, Ulaya na India.

Malaysia ina chimbuko lake kwenye falme ndogondogo za Wamalay zilizopo katika eneo hilo, ambalo, kuanzia karne ya 18, liliwekwa chini ya himaya ya Uingereza. Malaysia ni nchi ya makabila na tamaduni mbalimbali, ambazo zinatoa mchango mkubwa katika siasa. Karibu nusu ya wakaazi wa taifa hilo ni wa kabila la Wamalay, na kuna idadi kubwa ya Wamalaysia wenye asili ya China, ambao pia wanaunda jamii ya pili kwa ukubwa ya Wachina walioko ngambo duniani. Katiba ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu lakini inautambua Uislamu kuwa dini rasmi. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu Malaysia.

Onesha makala zaidi