LAGOS : Mashtaka dhidi ya Atiku yatupiliwa mbali | Habari za Ulimwengu | DW | 29.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS : Mashtaka dhidi ya Atiku yatupiliwa mbali

Mahkama ya Nigeria imetangua hatua za kisheria dhidi ya Makamo wa Rais wa nchi hiyo Atiku Abubakar kwa madai ya rushwa na kumwezesha kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Mahkama Kuu ya Lagos imepitisha hukumu hiyo leo hii kwa kusema kwamba repoti mbili juu ya Abubakar moja ya Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha inayomshutumu kwa kutumia vibaya fedha za umma na nyengine ya jopo la mawaziri yenye kusema anapaswa kushtakiwa kwa rushwa hazina msingi wa kisheria.

Hukumu hiyo inamaanisha kwamba repoti hizo haziko kisheria kwa hiyo makamo wa rais huyo yuko huru dhidi ya kikwazo chochote kile cha sheria kuwania urais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com