Kinyanganyiro cha kufuzu Kombe la Dunia 2010 | Michezo | DW | 31.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kinyanganyiro cha kufuzu Kombe la Dunia 2010

Ujerumani ina miadi leo na Wales:Brazil kesho na Peru.

Kocha Loew na nahodha Ballack.

Kocha Loew na nahodha Ballack.

Baada ya duru ya mwishoni mwa wiki iliopita timu za kanda ya ulya,Amerika ya kati na kusini na hata Asia, zinarudi uwanja ni leo na kesho kuan ia tiketi zao kwa finali ya Kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini 2010.

Ujerumani iliojipatia mteremko mbele ya Liechtenstein wa mabao 4:0 jumamosi, lio wanapanda mlima na Wales kabla ya changamoto yao na urusi hapo oktoba kuamia nani ataparia kileleni mwa kundi lao la 4 na kutia mfukoni tiketi ya kombe la dunia,la kwanza barani Afrika.

Uchunguzi umeanzishwa na washtaki wa serikali nchini ivory Coast jana juu ya vurumai iliozuka uwanjani jumapili pale tembo wa Corte d-Iviore walipowakanyaga Malawi kwa mabao 5-0 na mashabiki 22 kuuwawa ukuta wa uwanja ulipoporomoka.

Ujerumani leo ikiwa na miadi na Wales, imeazimia kuonesha mchezo tofauti na ule wa jumam osi walipowaonea chipukizi wa Liechtenstein na kuwazaba mabao 4-0.Wanahitaji pointi 3 nyengine leo ili kutia mfukoni pointi 6 kabla ya miadi yao itaklayowatoa jasho na Urusi hapo oktoba.Tangu Ujerumani kupokonywa taji la Ulaya na Spain,mwaka jana ufa umeingia katika kikosi chake .

Imelazwa mapambano 2 yaliofuatia-kwanza na waingereza kwa mabao 2-1 na halafu na wanorway kwa bao 1:0.

Mpambano wa leo utaonesha iwapo ufa huo umeanza kuzibwa.Nahodha Michael Ballack alielifumania kwanza lango la Liechtenstein jumamosi iliopita, anadai Ujerumani lazima irudie mchezo wake wa kucheza kwa nguvu na kasi ikiwa iantaka kurejea kutamba. Ujerumani itategemea tena leo washambulizi wake akina Lukas Podolski na Gomez ,kwani Miroslav Klose ameumia. Schweinsteiger,pia wa kutegemewa kutia magoli.

Uingereza iliomuita uwanjani Darren Bent kujaza pengo la mshambulizi Emile Heskey na Carlton Cole kwa miadi ya leo na Ukraine ameumia na sasa .

Kocha wa Uingereza mtaliana Fabio Capello,amemteua pia Gabriel Abonlahor wa aston villa, kujaza pengo lake.

Heskey aliumia baada ya England kuitimua nje Slovakia kwa maba 4:0 jumamosi iliopita.

Wadachi-Holland wanaelekea kutoroka na tiketi yao ya kombe la dunia 2010 huko Afrika kusini,mradi tu wamekiuka kizingiti cha leo macedonia.Ushindi leo mjini The Hague ,utaisukuma holland karibu sana kuondoka na tiketi ya Afrika.

Katika kanda ya Amerika Kusini, Brazil ina miadi kesho alhamisi na Peru wakati mahasimu wao wakubwa katika kanda ya Amerika kusini Argentina ikiongozwa na kocha Maradona,inacheza mjimni La Paz na bolivia.Venezuela inaumana leo na Columbia.

Mchezaji wa zamani wa mwaka wa dunia na ulaya Kaka ,yumkini akaitwa kulikoa jahzi la Brazil lisiende mrama na mwishoe kuzama katika dharuba na Peru hapo kesho.Ingawa Brazil daima inakata tiketi yake ya kombe la dunia, Brazil hadi sasa imeshinda mechi 4 kati ya 11 za kufuzu kombe la dunia.Jumapili iliopita Brazil imudu sare tu na chipukizi Ecuador.Kaka aweza kugeuza mkondo huu-aonavyo kocha dunga.

Taarifa kutoka Abidjan,zinasema kuwa, washtaki jana wameanzisha uchunguzi juu ya visa vilivyopelekea kufariki dunia kwa mashabiki 22 wa dimba jumapili iliopita mjini Abidjan,pale Tembo wa Core d-Ivire walipotamba uwanjani na kuwakanyaga wamalawi kwa mabao 5-0.Uchu wa mashabiki wa kupita kiasi kwa mpambano huo ,uliongoza kuelemea ukuta na ukaporomoka huku mashabiki wakikanyagana katika vurumai iliofuata.

Rais Laurent Gbagbo ,amesema amemtaka Raymond Tchimou -mshtaki wa serikali mjini Abidjan, kuanzisha uchunguzi haraka kujua sababu ya msiba wa jumapili.

Muandishi:Ramadhan Ali

Mhariri: Josephat Charo