Kinyanganyiro cha Kombe la dunia 2010 | Michezo | DW | 27.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kinyanganyiro cha Kombe la dunia 2010

Kanda ya ulaya na Afrika uwanjani.

** Nahodha wa Ujerumani ballack na kocha Loew

** Nahodha wa Ujerumani ballack na kocha Loew

Mashabiki wa simba wa nyika Kamerun na Super eagles -Nigeria, watazamia timu zao leo zitatamba ili kukata tiketi ya kombe lijalo la dunia mwakani nchini Afrika Kusini.

Ujerumani nayo ina miadi jioni hii na Liechtenstein kabla haikupambana na Wales jumatano ijayo kwa tiketi ya kombe hilo la dunia-

Uingereza imetoa rasmi ombi lake kutaka kuandaa kombe la dunia ama 2018 au 2022.

Mbio za magari za Fomular one,zarudi barabarani kesho kwa msimu mpya huko Australia.

Tuanze na ki nyanganyiro cha leo cha kuania kufuzu kwa Kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini kanda ya Ulaya:

Mshambulizi wa Bayern Munich,atakaerejea klabu yake ya zamani FC Cologne, mwishoni mwa msimu huu Lukas Podolski,anateremshwa uwanjani leo Ujerumani ikicheza na Liechtenstein kuipatia Ujerumani pointi 3 inazohitaji kabla kluvaana jumatano ijayo na Wales kuhakikisha inanyakua tiketi yake ya Kombe lijalo la dunia.Mshambulizi huyu alieachwa nje ya kikosi cha Taifa pale Ujerumani ilipocheza mapambano 2 ya kirafiki na Uingereza na Norway na kushindwa yote mawili.

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew anamhitaji leo podolski kuipiga kumbo Liechtenstein huko Leipzig na jumatano ijayo itapocheza na Wales kabla zahyama kali zaidi na Urusi hapo oktoba.Mshambulizi wa Ujerumani Miroslav klose ameumia na katika ngome ya ujerumani, Arne Friederich wa Hertha berlin pia anachchemea nje ya chaki ya uwanja .Rene Adler kipa wa Leverkusen aliejaza pengo la Oliver Kahn hayuko fit,lakini huenda akalinda lango.Hatahivyo, Ujerumani inaongoza kundi lake la 4 wakati huu ikiwa na jumla ya pointi 10 ikifuatwa na urusi na Wales ambazo kila moja ina pointi 6.Mshindi wa kila kundi anatia mfukoni tiketi yake ya kushiriki Kombe la dunia.

Mabingwa wa dunia-Itali ,wakiongozwa tena na kocha wao Marcello Lippi hawamudu pigo jengine baada ya lile waliopewa na mabingwa wa Amerika kusini-Brazil mwezi uliopita wsalipochapwa mabao 2:0 . Itali ina miadi leo na Montenegro.Wakishindwa kutamba, Squad Azzurri,huenda isitetee taji lake mwakani Afrika kusini.Lippi ameangusha majabali mengi na anadai hatashindwa na hili.

Kanda ya Afrika halkadhalika ,inaendelea na kinyanganyiro chake cha kuamua ni timu gani 5 zitajiunga na wenyeji Afrika kusini Juni mwakani kuania kombe la dunia. Jayson Nyakundi anawafungulia pazia upande huo:

JAYSON NYAKUNDI:

Kwa mashabiki wa simba wa nyika-Kamerun na Super Eagles Nigeria, hawataweza kuvumilia pigo jengine na kuzikosa kuziona timu zao 2 katika Kombe lijalo la dunia Afrika kusini,Juni mwakani. 2006 Kombe hilo la dunia lilipoaniwa Ujerumani, Ivory Coast ili ipiku Kamerun na kuja Ujerumani kwa mara ya kwanza katika Kombe la dunia.Nigeria, ilishindwa kutamba katika kundi lake na Angola.

Nigeria imekamia kushinda katika kundi lake mara hii ,lakini kesho jumapili haina mtremko bali kibarua kigumu mjini Maputo ili kuweza mwishoe kutamba kundi B.

Nigeria sio tu itapaswa kuwatimua baadae Harambee Stars (Kenya) wenye miadi leo na Tunisia, bali pia Msumbiji wakielewa kasoro ya ushindi mjini Maputo kesho ,haitatosha.kwani,Nigeria lazima iparamie mnazi hadi kileleni na kuipiku Tunisia.

Wenzao "The Eagles of Carthage" kama timu ya Tunisia inavyojulikana, wamepania leo kutamba juu ya anga la Nairobi mradi tu Kenya Airways itaruhusu .

Kwa simba wa nyika-Kamerun kushindwa kushiriki katika Kombe lililopita la Dunia hapa Ujerumani, ilikua madhambi makubwa kwa mashabiki wake tangu wa nyumbani hata Afrika.Katika mpambano wao wa mwisho,simba wa nyika walitznukiwa mkwaju wa adhabu wa penalty katika lango la Misri:laiti,Pierre Wome angetia bao,simba wanyika wangekuja Ujerumani kunguruma 2006,lakini wapi,ilikuwa tembo wa Ivory Coast waliokuja kukanyaga nyasi.

Leo kocha wao mjerumani Otto Pfister,amewasili nna simba wa nyika porini Lome kwa miadi na Togo-timu ilionja utamu wsa kucheza katika kombe lililopita la dunia na inataka tena-kwani wanasema" Mramba asali-harambi mara moja."

Kamerun na Togo zinakabili upinzani mkali kwa tiketi yao kutoka simba wa Atlas-Morocco wanaocheza nyumbani na Gabon.

Malawi imefunga safari hadi Abidjan kwa kivumbi na Tembo wa ivory Coast katika changamoto ambayo hakuna anaetazamia timu hii kutoka Afrika mashariki kushinda.Hatahivyo, mpira wanasema unadunda na huenda ukakurejea.Kuna timu nyengine mbili za Afrika magharibi zinazoonana:Burkina Faso na Guinea.Miadi yao ni Ougadogou.

Katika kundi C,timu mbili zinazotazamiwa kluja juu ni mabingwa wa afrika -mafiraouni Misri na (Chipolopolo au risasi) Zambia. Risasi za Chipolopolo zitakuwa n a kazi ngumu kutoboa ukuta wa ngome ya mafiraouni mjini Cairo.

Rwanda inadai haina wasi wasi nyumbani ingawea inatembelewa na waakilishi wa zamani wa kombe la dunia-Algeria.

Kwa desturi washindi wa makundi hayo 5 ya kanda ya Afrika ,watajiunga na wenyeji wa Kombe lijalo la dunia-Bafana Bafana -Afrika kusini Juni,mwakani kuteremsha uwanjani timu 6 za Afrika kwa vita vya kulibakisha kmombe kwa mara ya kwanza nyumbani Afrika.

Timu 3 za usoni kutoka kila kundi,zitakataa tiketi zao kwa finali ya kombe la Afrika la mataifa nchini Angola,litakalofungua pazia mwaka huu kwa Kombe la dunia,upande wapili wa mpaka-Afrika kusini.

Tukibakia katika mada ya kombe la dunia,taarifa kutoka Johannesberg zinasema Afrika kusini, ikiwa wenyeji wa kombe lijalo na Brazil,wenyeji wa kombe la dunia 2014 w zimeamua kushirikiana.Waziri wa ulinzi wa Afrika kusini, Charles Ngakula amenukuliwa kusema kuwa juhudi zimechukuliwa na Brazil,India na Afrika kusini kutunga mkakati bora wa kukabiliana na vitisho juu ya usalama . Swali la usalama na uhalifu, limekuwa mojawapo ya wasi wasi wakati wa kombe la dunia.

Mwezi uliopita Mkuu wa polisi wa Munich,Ujerumani, Wilhelm Schmidbauer,

alizuru Afrika Kusini kuzungumzia mahitaji ya Afrika kusini wakati wa kombe la dunia na vipi vyombo vya usalama vya Bavaria na Afrika kusini ,vyaweza kushirikiana 2010.

Na wakati wa zaiara yake hiyo fupi,binafsi, alilengwa na wevi huko Cape Town. Gari alilopanda Schmidbauer lilizingirwa na vijana baada ya kukitembelea kituo cha polisi.Vijana hao walijaribu kufungua mlango wa gari hilo na sehemu ya nyuma. Pale dereva wake alipogundua kinapita nini,alitimka mbio na gari lake.

Hatahivyo, wakuu wa Afrika Kusini, wameendelea kudai kuwa usalama utakuwapo mwakani wakati wa kombe la dunia.Juni hii,wiki chache kutoka sasa, Kombe la Mashirikisho-Confederations Cup likiingiza mabingwa wa kanda zote,litafungua pazia la Kombe la dunia na tutaona hali ya usalama itakuaje.

Chama cha mpira cha Uingereza-FA wiki hii , kilitoa ombi lake rasmi kuandaa Kombe la Dunia la dimba ama 2018 au 2022.Uingereza , inatoa changamoto kwa Australia,Indonesia,Korea ya KusiniUrssi,Qatar,Mexico na hata Marekani.

Mara ya mwisho Uingereza kuandaa Kombe la dunia ilikuwsa 1966 ilipoilaza Ujerumani na kuvaa taji la dunia.

Mbio za magari za "formular One", zaanza msimu wsake mpya kesho huko Australia na magari ya Williams , yameshatoa salamu jana kuwa yanatakata kutamba:

Nico Rosberg wa magari ya Williams ndie alietia fora katika mazowezi ya siku ya kwanza wakati bingwa wa dunia muingereza Lewis Hamilton wa magari ya M cLaren ,akiburura mkia.Muhimu nani kesho atatoa salamu za mwaka mpya za mbio za formular-one kwa mwenzake .

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: A.Liongo