Kimbunga Xynthia kimeua watu 56 barani Ulaya | Masuala ya Jamii | DW | 01.03.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kimbunga Xynthia kimeua watu 56 barani Ulaya

Watu 56 wameuawa katika kimbunga kilichopiga siku ya Jumapili magharibi ya Ulaya. Upepo uliofikia mwendo wa kilomoita 175 kwa saa umengóa miti na minara ya umeme na kusababisha watu kukaa gizani.

Collage Überschwemmung in Aytre in Frankreich am 28.02.2010 (AP) / Sturmschäden in Saarbrücken (apn) / Montage: DW

Picha mbili zaonyesha uharibifu uliosababishwa na kimbunga Xynthia katika mji wa Aytre,Ufaransa.

Kimbunga hicho kilichoitwa Xynthia kilitokea Bahari ya Atlantik na kikapiga katika pwani ya magharibi ya Ufaransa na Uhispania kabla ya kuendelea hadi Ureno, Uholanzi na Ujerumani. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy hii leo anatembelea eneo la pwani lililoathirika vibaya zaidi. Kimbunga kilichofikia mwendo wa kilomita 175 kwa saa na mawimbi ya urefu wa mita nane yamesababisha mafuriko hadi katika maeneo ya ndani na watu walipaswa kukimbilia kwenye mapaa ya nyumba.

Umgestuerzte Baeume sind am Sonntag, 28. Februar 2010, in der Wiedfeldstrasse in Essen zu sehen. Chaos auf Strasse und Schiene, zahlreiche Ausfaelle im Flugverkehr und dazu mindestens ein Toter - Sturmtief Xynthia hat am Sonntag auch Deutschland erfasst. Die Meteorologen rechneten mit Windgeschwindigkeiten bis zu 120 Stundenkilometern. (apn Photo/KDF-TV, Stephan Witte) ** zu APD2958 ** --- A crashed tree lays across a street in Essen, Germany, after being uprooted by gale force storm Xynthia on Sunday, Feb. 28, 2010. (apn Photo/KDF-TV, Stephan Witte)

Miti iliyoangukia barabarani mjini Essen,Ujerumani.

Dhoruba hiyo imeng'oa miti na minara ya umeme, na mamilioni ya watu wamebakia bila ya umeme hasa katika eneo la pwani la Brittany. Kwa mujibu wa shirika la umeme la Ufaransa EDF, hali hiyo huenda ikaendelea kwa siku kadhaa. Hata misafara ya ndege na treni imevurugwa na maelfu ya abiria walinasa katika stesheni za treni na kwenye viwanja vya ndege.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Francois Fillon amesema, atatangaza kimbunga hicho kuwa ni maafa ya kimaumbile na kutatolewa fedha maalum kusaidia kazi za ukarabati katika jamii. Ufaransa itawasilisha maombi yake katika Umoja wa Ulaya kupatiwa fedha hizo kutoka fuko maalum ili kusaidia operesheni za ukarabati. Nchini Ufaransa pekee imethibitishwa kuwa watu 47 wameuawa na wengine 30 hawajulikani walipo.

Kimbunga Xynthia kilifika Ujerumani,Ubeligiji na Uholanzi Jumapili mchana na kikaendelea kuvuma hadi usiku na kuvuruga misafara ya treni na ndege. Huku Ujerumani watu wawili walipoteza maisha yao baada ya kuangukiwa na miti. Na Uhispania pia wanaume wawili waliokuwa katika gari waliuawa walipoangukiwa na mti na nchini humo humo mwanamke mmoja mzee alifariki baada ya kuangukiwa na ukuta.

Nchini Ujerumani, shirika la treni Deutsche Bahn jana jioni lililazimika kufuta safari nyingi kwa sababu ya miti iliyoangukia njia za reli. Waokozi wamefanya kazi usiku mzima kuhakikisha shughuli za usafiri zinaanza kufanya kazi. Kimbunga Xynthia sasa kinaelekea kaskazini ya Ulaya.

Mwandishi: P.Martin/AFPE/DPA

Mhariri: Othman,Miraji

 • Tarehe 01.03.2010
 • Mwandishi Prema Martin
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MEsE
 • Tarehe 01.03.2010
 • Mwandishi Prema Martin
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MEsE
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com