KENNEBUNK PORT:Bush, Putin wakubaliana juu ya Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KENNEBUNK PORT:Bush, Putin wakubaliana juu ya Iran

Rais George Bush wa Marekani na mgeni wake Vladmir Putin wa Urusi wamesema kuwa watashirikiana katika kutatua mzozo wa mpango wa nuklia wa Iran.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao huko Kennebunkport, Rais Bush, alisema kuwa ana imani Urusi itaunga mkono katika kutuma ujumbe wa tahadhari kwa Iran kupitia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Bush alielezea wasi wasi juu ya mpango huo wa nuklia wa Iran.

Lakini viongozi hao walishindwa kuondoa tofauti zao juu ya mapngo wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami katika nchi za Poland na Jamuhuri ya Czech.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com