Kashfa ya Ufisadi yawakumba mawaziri nchini Uganda
2 Septemba 2008
Nchini Uganda Waziri wa usalama wa Taifa wa nchi hiyo Amama Mbabazi pamoja na Waziri wa Fedha Dr Ezra Suruma wako katika mbinyo mkubwa wa kujiuzulu baada ya kuhusishwa na kashfa ya ufisadi.
https://p.dw.com/p/FAAq
Matangazo
Kashfa hiyo inatokana na Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi nchini Uganda NSSF kununua ardhi kutoka kwa Waziri Mbabazi katika mazingira yenye harufu ya rushwa.
Kutoka Kampala Kigozi Ismail ametutumia taarifa ifuatayo.