Karadzic huenda akafikishwa mahakama ya The Hague wiki ijayo | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Karadzic huenda akafikishwa mahakama ya The Hague wiki ijayo

-

BELGRADE

Wakili wa mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita Radovan Karadzic amesema mteja wake huenda akafikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita mjini The Hague jumatano au alhamisi wiki ijayo.

Hata hivyo wakili huyo amekataa kutoa maelezo juu ya taarifa kwamba amekata rufaa dhidi ya mteja wake kufikishwa The Hague dakika za mwisho kabla ya kumalizika muda wa kufanya hivyo ijumaa usiku.

Wakati huohuo maelfu ya wanaomuunga mkono Karadzic waliandamana jana kupinga kukamatwa kwake na hatua ya kutaka kumfikisha The Hague.

Maandamano hayo yalifanyika kote katika eneo la Serbia upande wa Bosnia na hasa kwenye mji wa Pale ambako Karadzic alikuwa na makao makuu yake wakati wa vita vya mwaka 1992 hadi mwaka 1995.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com