KARACHI: Tufani na mafuriko yaua zaidi ya 200 Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 26.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARACHI: Tufani na mafuriko yaua zaidi ya 200 Pakistan

Zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha yao katika tufani na mvua kubwa zilizonyesha katika jiji kubwa kabisa nchini Pakistan,Karachi.Umeme ulikatika sehemu nyingi za mji wa Karachi na wakazi waliohamakishwa walichoma moto mipira ya gari barabarani na walitupia mawe magari yaliokuwa yakipita njiani.Mtu mmoja aliuawa katika ghasia hizo.Kwa mujibu wa idara ya kutabiri hali ya hewa,mvua zaidi zinatazamiwa kunyesha nchini Pakistan na nchi ya jirani ya India ambako watu darzeni kadhaa wamepoteza maisha yao katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha nchini humo siku chache zilizopita.Helikopta za kijeshi na wafanyakazi wa mashirika ya misaada,wanajitahidi kuwapelekea chakula kiasi ya watu 200,000 waliolazimika kuondoka makwao kwa sababu ya mafuriko ya msimu wa masika,katika jimbo la Andhra Pradesh kusini mwa India.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com