1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Karl Marx

Karl Marx (1818-1883) alikuwa mwanafalsafa mzaliwa wa Ujerumani wa karne ya 19 ambaye kazi zake zilihusisha nadharia za kiuchumi, sosholojia na siasa na baadae zilikuja kubadili siasa katika mataifa mengi duniani.

Karl Marx ambaye alizaliwa katika mji wa Trier, alikimbilia nchini England na kukosa utaifa mwaka 1849, baada ya kuonekana tishio la kisiasa nchini Ujerumani. Akijulikana kama "baba wa ukomunisti", aliandaika kabrasha la kisiasa la "The Communist Manifesto" au "Ilani ya kikomunisti" (1848) na Friedrich Engels, na ndiye mwandishi wa matini ya msingi wa nadharia ya "Capital: Critique of the Political Economy" au "Tajiriba: Tahakiki ya Uchumi wa Kisiasa." (1867-1883).