1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz ziarani Kenya

Grace Kabogo
5 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz leo anaendelea na ziara yake barani Afrika, kwa kuitembelea Kenya na kufanya mazungumzo ya kisiasa.

https://p.dw.com/p/4QwZA
Berlin Präsident William Ruto Kenia und Kanzler Scholz
Picha: Political-Moments/IMAGO

Scholz ambaye tayari amewasili mjini Nairobi, anakutana na mwenyeji wake Rais William Ruto. Scholz pia atazungumzia matumizi ya nishati jadidifu, utatuzi wa migogoro ya kikanda na upanuzi wa uhusiano wa kiuchumi.

Serikali ya Ujerumani inaichukulia Kenya kama mshirika wake muhimu zaidi wa kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Soma zaidi: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aelekea Ethiopia na Kenya katika ziara yake ya pili barani Afrika.

Pia inaiona Kenya kama nchi ya mfano mwema kwa Afrika Mashariki linapokuja suala la utawala wa kidemokrasia.

Scholz alianza jana ziara yake ya siku tatu barani Afrika, kwa kuizuru Ethiopia, ambapo alikutana na viongozi wa serikali na wa Umoja wa Afrika.