1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yatakiwa kuongeza nguvu zaidi kwenye ulinzi

28 Januari 2026

Mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema, Ulaya inapaswa kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi mara moja kutokana na uhusiano wa mashaka kati ya Umoja huo na Rais wa Marekani Donald Trump.

https://p.dw.com/p/57as1
Umoja wa Ulaya umetakiwa kuongeza nguvu katika sekta ya ulinzi
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja KallasPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Kallas Ameyasema hayo katika mkutano wa ulinzi unaofanyika mjini Brussells. Ameeleza kuwa Ulaya inapaswa kukubaliana na uhalisia mpya kwani siyo tena eneo kuu linalotegemewa na Washington.

Kitisho cha kuinyakua Greenland ni tahadhari kwa Ulaya

Mkuu huyo wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ametoa kauli hiyo wiki kadhaa baada ya Trump kutishia kuinyakua Greenland kutoka kwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kutoka kwa Denmark ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Nchi za umoja huo zimeshaongeza bajeti zao za Ulinzi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine. Zilikubaliana pia kuongeza bajeti ya ulinzi katika Jumuiya ya NATO kutokana na shinikizo la Trump.