KABUL:Mkutano juu ya usalama baina ya Pakistan na Afghastan kuendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Mkutano juu ya usalama baina ya Pakistan na Afghastan kuendelea

Baraza la amani linalowajumuisha viongozi wa kisiasa na kikabila kutoka Pakistan na Afghanstan limeanza mkutano wake katika mji mkuu wa Afghanstan Kabul.Kikao hicho kilianza kufunguliwa kwa dua maalum za kumuomba mwenyezi mungu. Rais wa Pakistan Pervez Musharaf aliyetazamiwa kuhudhuria mkutano wa leo aliamua dakika za mwisho kutohudhuria na badala yake kuwakilishwa na waziri mkuu Shaukat Aziz. Waziri mkuu huyo ameandamana na kiasi cha wajumbe wa serikali 175 pamoja na wawakishi wa makabila.Rais Hamid Karzai akiufungua mkutano huu aliwaambia wajumbe 700 waliohudhuria kwamba hatma ya Afghanstan na Pakistan inaangaliwa na kwamba pamoja wanaweza kuushinda udhalimu.

Vipi tunaweza kuwashinda wataliban hilo ndilo swali la msingi ambalo ni lazima tulitafutie jibu.

Hali ya usalama imeimarishwa ambapo kiasi maafisa 2500 wapolisi wanalinda mkutano huo maarufu Jirga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com