KABUL: Raia wauawa katika mashambulizi ya kujitolea muhanga | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Raia wauawa katika mashambulizi ya kujitolea muhanga

Raia mmoja ameuawa na wengine 6 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa karibu na msafara wa magari ya majeshi ya Marekani,kaskazini mwa Afghanistan.Mripuko huo umetokea mji wa Mazar-i-Sharif saa chache tu baada ya mshambulizi aliejitolea muhanga ndani ya gari lenye bomu,kushambulia msafara wa walinzi wa usalama wa kigeni mjini Kabul.Katika shambulio hilo raia 3 wa Afghanistan waliuawa na wengine 5 walijeruhiwa.Kufuatia shambulio la mjini Kabul,vikosi vya Marekani vilifyatua risasi miongoni mwa umma na kusababisha kifo cha raia mmoja na kuwajeruhi wengi wengine.Kwa mujibu wa majeshi ya Marekani hayo yametokea kwa kosa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com