KABUL: Hakuna maafikiano ya mahala pa kukutana na Taliban | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Hakuna maafikiano ya mahala pa kukutana na Taliban

Wanamgambo wa Taliban wamesema,hakuna makubaliano yaliyopatikana juu ya mahala pa kufanywa mkutano wa ana kwa ana pamoja na wanadiplomasia wa Korea ya Kusini.Wanadiplomasia hao wanajaribu kupata uhuru wa raia wenzao 21 waliotekwa nyara majuma mawili yaliyopita.Ujumbe wa Korea ya Kusini ulikuwepo wilaya ya Ghazni,kusini-magharibi ya mji mkuu wa Afghanistan,Kabul kujaribu kukutana uso kwa uso na wateka nyara.

Wataliban wanataka majadiliano hayo yafanywe katika eneo wanalodhibiti au wahakikishwe usalama wao,ikiwa mkutano huo utafanywa kwengineko. Wataliban wameshawaua mateka 2 na wametishia kuwaua wote wengine,pindi serikali ya Afghanistan haitowaachilia huru waasi walio jela.

Wakati huo huo,Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani,inaendelea na jitahada za kupata uhuru wa mhandisi wa Kijerumani aliezuiliwa pia na wanamgambo wa Taliban.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com