JERUSALEM: Mkutano kuhusu mashariki ya kati wamalizika bila taarifa ya pamoja | Habari za Ulimwengu | DW | 26.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Mkutano kuhusu mashariki ya kati wamalizika bila taarifa ya pamoja

Mkutano wa wapatanishi wa mzozo wa mashariki ya kati umalizika mjini Jerusalem bila kutolewa taarifa rasmi ya pamoja.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema mjumbe wa umoja huo wa mashariki ya kati, Marc Otte, atawasilisha makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo mjini Brussels kabla taarifa ya pamoja kutolewa.

Mazungumzo ya leo yanafungua mlango kwa waziri mkuu wa Uingereza anayeondoka, Tony Blair kuteuliwa kama mjumbe maalumu wa mashariki ya kati kwa niaba ya pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya eneo hilo, zikiwemo Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Urusi.

Blair atatangazwa rasmi hivi karibuni kuanza kazi hiyo, lakini kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza limesema halimtaki kwa sababu alihusika katika vita dhidi ya Irak na Afghanistan vilivyoongozwa na Marekani.

Mkutano wa mjini Jerusalem ni wa kwanza tangu kundi la Hamas lilipolidhibiti eneo la Ukanda wa Gaza na umefanyika siku moja baada ya viongozi wa Israel, Palestina, Misri na Jordan kuahidi kushirikiana kuufufua mchakato wa kutafuta amani ya Mashariki ya Kati kwenye mkutano uliofanyika huko Sharm el Sheikh nchini Misri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com