1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaikamata meli nyingine ya misaada

Sekione Kitojo5 Juni 2010

Israel imeikamata meli nyingine ya misaada iliyokuwa inaelekea Gaza siku nne baada ya kuvamia meli za misaada na kusababisha watu tisa kuuwawa.

https://p.dw.com/p/Nifm
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekasirishwa sana na hatua ya Israel kuzizuwia meli za misaada zilizokuwa zinaelekea Gaza, pamoja na kuuwawa kwa raia wanane wa nchi hiyo.Picha: AP

Israel inameikamata meli nyingine ya misaada iliyokuwa inaelekea Gaza, hatua inayozidisha wasiwasi zaidi kuhusiana na hatua ya Israel kulizingira eneo la Gaza linalotawaliwa na kundi la Hamas. Israel imekabiliwa na shutma za kimataifa baada ya operesheni yake ya Jumatatu, pale wanaharakati tisa wa Uturuki walipouawa ndani ya meli iliyokuwa inaelekea Gaza. Israel imesisitiza uamuzi wake wa kuendelea kulizingira kijeshi eneo la Gaza, baada ya kundi la Hamas kuchukua mamlaka, ni kuzuwia kuingizwa kwa silaha. Mjini Washington, Ikulu ya Marekani imesema hatua ya Israel kulizingira eneo la Gaza haina maana ya kuendelezwa lakini, pia Ikulu hiyo ikazihimiza meli za misaada zinazoelekea Gaza kuelekea katika bandari ya Israel ili kuzuia kutokea kwa rabsha.