1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapata shehena ya mafuta ya kinuklia.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdB8

Bushehr, Iran.

Urusi imepeleka shehena ya kwanza ya mafuta ya kinuklia kwa ajili ya kinu cha kinuklia ambacho nchi hiyo inasaidia kukijenga katika eneo la Bushehr. Mataifa makubwa ya umoja wa Ulaya pamoja na Marekani yanashaka kuwa Iran inatengeneza silaha za kinuklia. Iran imesema kuwa shughuli zake za kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani lakini imekataa madai ya kuitaka kuacha kazi ya kurutubisha madini yake ya uranium.

Utawala wa rais Bush hadi sasa umekuwa na wasi wasi juu ya Iran kumiliki madini ya uranium yaliyorutubishwa. Lakini msemaji wa Ikulu ya Marekani Gordon Johndroe amesema iwapo Urusi imeipatia Iran madini yaliyokwisha rutubishwa , hakuna haja tena kwa Iran kuendelea kurutubisha madini hayo yenyewe.