1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo katika mgodi China yafikia 105

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYit

BEIJING

Idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 105 kutokana na mripuko wa gesi kwenye mgodi wa makaa ya mawe kaskazini mwa China.

Wafanyakazi wengi wa mgodi wamekufa kutokana na sumu ya carbon monoxide kwa mujibu wa wafanyakazi wa uokozi kwenye eneo hilo la maafa.Juhudi za kuwatafuta wahanga zaidi zinaendelea.

Polisi imemkamata mmiliki na meneja wa mgodi huo kwa tuhuma za kusubiri kwa masaa sita kabla ya kurepoti mripuko huo wa gesi uliosababisha maafa ambao maafisa wanaoshughulikia taratibu za usalama wanatuhumu kwamba umetokea kutokana na kazi isio ya halali iliokuwa ikifanyika kwenye sehemu moja isiorohusiwa kufanya kazi kwenye mgodi huo.