1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong yapiga marufuku ndege kutoka nchi nane duniani

Saleh Mwanamilongo
5 Januari 2022

Maambukizi ya kirusi kipya cha omicron yameongezeka duniani. Hong Kong imetangaza marufuku ya  wiki mbili za safari za ndege zinazoingia kutoka nchi nane.

https://p.dw.com/p/45A35
Carrie Lam | Hongkong | Regierungschefin
Picha: Kyodo/picture alliance

Mamlaka huko Hong Kong imeimarisha vizuizi vya ndani katika kupambana na kirusi kipya cha omicron. Kiongozi wa HongKong, Carrie Lam amesema leo Jumatano kwamba ndege zinazoingia kutoka Autralia,Canada,Ufaransa, India,Pakistan, Ufilipino,Uingereza na Marekani ni marufuku.

''Kwa wale ambao wanaondoka kutoka nchi nyengine mbali na hizo nane, lakini wamewahi kwenda katika nchi hizi nane,pia hawataruhusiwa kupanda ndege (kwenda Hong Kong). Ni hatua kali inayotekelezwa hivi sasa.",alisema Lam.

Lam amesema kuanzia Ijumaa, serikali itapiga marufuku migahawa baada ya saa 12 jioni,vituo vya michezo, baa na vilabu, maeneo ya makumbusho, na kumbi nyinginezo kwa angalau wiki mbili.

Soma pia: Hali ya Maambukizi ya corona na ugonjwa wa COVID-19

Israel kuchukua hatua mpya

Licha ya vizuizi na marufuku ya safari za ndege kutoka nje, Israel leo imetangaza kurikodi idadi ya juu kabisa ya maamkukizi mapya ya Corona tokea janga hili kutangazwa miaka miwili iliyopita. Wizara afya ya Isreal imeripoti visa takriban 12 elfu mnamo muda wa masaa 24.

Nchini Ufaransa idadi ya maambukizi mapya ilifikia watu laki mbili na tisini elfu, katika kipindi cha masaa 24. Rais Emmanuel Macron Jumatano alikabiliwa na hasira kutoka kwa wapinzani na machafuko bungeni baada ya kutoa onyo kwa watu nchini Ufaransa ambao bado hawajachanjwa dhidi ya Covid-19 kwamba atawashinikiza iwezekanavyo kwa kuzuia ufikiaji wa nyanja muhimu za maisha.

Marekani yaonya ongezeko la maambukizi

Wataalamu wa afya Marekani waonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya visa vya corona
Wataalamu wa afya Marekani waonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya visa vya coronaPicha: CAP/MPI/RS ©RS/MPI/Capital Pictures/picture alliance

Marekani ilirekodi idadi ya juu zaidi ya watu milioni moja walioambukizwa virusi vya corona ndani ya siku moja. Mtaalamu ambaye pia ni mshauri mkuu wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani daktari Anthony Fauci, alisema nchi hiyo inakabiliwa na ongezeko kubwa la maambukizi na huenda hali hiyo itasalia hivyo kwa wiki chache zijazo.

Hapa nchini Ujerumani  Kansela Olaf Scholz anatarajia kukutana Ijumaa na viongozi wa majimbo yote 16 ya Ujerumani ili kupanga hatua mpya ya kupambana na maabukizi ya kirusi cha omicron. 

Uingereza ilirekodi zaidi ya visa 200,000 vya ziada kwa mara ya kwanza Jumanne, wakati Australia iliweka rekodi ya visa 50,000 za kila siku.

Soma pia :Wajerumani wazidi kupinga vizuizi vya COVID-19

Marufuku ya kanavali ya Rio

Straßenkarneval in Rio de Janeiro abgesagt
Picha: Fernando Frazão/Agencia Brazil/dpa/picture alliance

Mamlaka huko Rio de Janeiro nchini Brazil iliamua Jumanne kusitisha gwaride kubwa la kitamaduni la kanivali, ambayo kwa mara ya mwisho mwaka 2020 tamasha hilo iliwakusanya watu milioni saba.

Janga hili la Covid-19 limewauwa watu wasiopungua 5,448,314 duniani kote tangu kuzuka Desemba 2019, kulingana na makadirio ya vyombo vya habari.