1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya seneta Obama Ikulu

29 Oktoba 2008

Njama ya kutaka kumua Obama ndio mada ya usoni leo hii:

https://p.dw.com/p/Fjb4
Obama alipokua chuo kikuu.Picha: AP

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani umetuwama leo juu ya mada moja hasa:juu ya njama ya kutaka kumuua mtetezi wa kiti cha urais nchini Marekani-seneta Obama kutokana na chuki za ukabila.Lakini pia safu za wahariri zinachambua msukosuko wa uchumi ulioikumba Pakistan na haja iliotambuliwa na serikali ya Ujerumani ya kuuchangamsha uchumi ili urejee kustawi.

Gazeti la NORDSEE-ZEITUNG kuhusu njama dhidi ya seneta Obama.Laandika:

"Tumshukuru Mungu shabaha ya wabaguzi hao 2 Manazi wa kimarekani haikufanikiwa.Hatahivyo, baadhi ya vyombo vya habari vinaitoa maanani njama hiyo kana kwamba ,waandazi wakipanga kutumia bastola bandia.Vyombo hivyo vya habari vinafumbia macho ukweli kuwa licha ya seneta Obama kuongoza wazi usoni katika uchunguzi wa maoni na ushindi wake umebashiriwa, sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani bado ina ubaguzi..

Kutoaminiana na dhana potofu kati ya wamarekani-weupe na wamarekani-weusi , kumesalia bado kwa kiwango kikubwa.Na hasa katika mashina ya wahafidhina ya Amerika ya kati,mawazo ya Obama yanakumbana na vichwa-mchungwa. Mawazo ya ukabila yaweza kumshawishi mpumbavu yoyote alieambukizwa dhana mbovu kutumia nguvu."

Ama gazeti la Rhein-Zeitung linasema ushindi kwa Obama sio tu kuipa kisogo miaka 8 ya utawala wa Bush, bali zaidi utakua tokeo la kihistoria.Gazeti laongeza:

Kwa kumchagua Obama, Marekani itaonesha imeufunga kabisa ukurasa wake wa chuki za kikabila na kuuzika kabisa.Pia itakua imeweka alama itakayoonekana wazi na kila muamerika-mweusi ambae bado hakuamini amani na wazungu imefikiwa.Sijui balaa gani lingetokea,endapo matumaini haya amani yangeteketezwa na wauaji waliovinjari kabisa.

Gazeti la Pfozheimer Zeitung likitumalizia mada hii kwa sasa laandika:

"Haikuwa sadfa tu ,kuona nchini Marekani ,hakuwahi kutawazwa kitini rais mweusi.Sababu yake yadhihirika ni ubaguzi wa kikabila kama ulivyobainishwa na vijana hao 2 waliotaka kumuua Obama ,ingawa mara hii yaonesha hali ni tofauti kidogo. kisichokatalika lakini, ni kua kuna raia wengi wa Marekani ambao kutokana na nadharia zao hawakubali kamwe muamerika mweusi kuwa rais wa M arekani. Wale wanaodhani hivyo,wanaweka siri yao moyoni.

Ndio maana licha ya uchunguzi wa maoni kubashiri ushindi wazi wa seneta Obama,bado si dhahiri kuwa seneta Obama mlngo tayari uwazi kuingia Ikulu.Moja lakini ni bayana:Ikiwa atafanya mapinduzi hayo na kuingia Obama Ikulu,usalama wake uko hatarini zaidi kuliko wa marais wote wale waliomtangulia."

Likitugeuzia mada,gazeti la Sąchsische Zeitung kutoka Dresden lauchambua msukosuko wa kiuchumi ulioikumba Pakistan hivi sasa.Laandika:

"Pakistan iko hatarini kuporomoka ikiwa jamii ya kimataifa haitaitia jeki na kuipatia mabilioni ya dala.Kwa Pakistan sio kuyaokoa mabanki nchini,bali kuokoa utulivu na kuimarisha nchi muhimu yenye silaha za kinuklia.

Kundi la marafiki wa Pakistan -Umoja wa Ulaya ,Marekani,Nchi za Ghuba na China- limekuwa na uwezo ingawa sio mkubwa sawa na huo katika kukabiliana na msukosuko wa fedha .Nchi hizo katika hali ya kufadhahika inayojikuta Pakistan,zitapaswa kutia raslimali zao huko.Serikali ya Pakistan inaelewa kuwa marafiki zake hawataiacha mkono hata ikiwa matatizo ya nchi hiyo kwa msaada huo hayatamalizika."