Hali ya kisiasa visiwani Zanzibar
21 Januari 2010Matangazo
Katika mahojiano yake na Aboubakary Liongo, Balozi Karume amesema muafaka uliofikiwa kati ya Rais Karume na Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ni suala ambalo alilipigia kelele hadharani lifanyike miaka miwili iliyopita na kujinasibu kuwa yeye ni sheikh Yahya Hussein wa siasa, akimaanisha yule mtabiri wa masuala ya siasa.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
Mhariri:Othman Miradji