GUANTANAMO :Mfungwa wa Guantanamo apewa kifungo cha miezi 9 | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GUANTANAMO :Mfungwa wa Guantanamo apewa kifungo cha miezi 9

Muaustralia aliezuiliwa na jeshi la Marekani katika jela ya Guantanamo Bay amehukumiwa kufungwa jela kwa kipindi cha miezi tisa.David Hicks alie na umri wa miaka 31,hapo awali alikubali makosa ya kusaidia ugaidi.Mahakama ya Kijeshi kwanza ilipendekeza kumpa kifungo cha miaka saba,lakini kwa sababu Hicks hapo kabla alikubali kukiri makosa,sasa hatofungwa zaidi ya miezi tisa.Hicks vile vile amekubali kufuta madai yake kuwa aliteswa alipozuiliwa na Marekani.Hicks ambae ameslimu,alikamatwa nchini Afghanistan mwaka 2001 akishukiwa kuhusika na ugaidi.David Hicks ni mfungwa wa kwanza kufikishwa mahakamani na kukutikana na hatia katika Mahakama ya Kijeshi ya Marekani.Hicks atatumikia kifungo hicho nchini mwake Australia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com