GAZA : Watano wauwawa katika mapigano ya Hamas na Fatah | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA : Watano wauwawa katika mapigano ya Hamas na Fatah

Mashambulizi ya risasi yameuwa takriban watu watano leo hii katika maandamano ya kundi la Fatah ya kumbukumbu ya miaka mitatu tokea kufariki kwa aliekuwa kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat ambayo yamehudhuriwa na mamia ya wafuasi wa kundi hilo lililoshindwa na kundi la Hamas katika mapambano ya kudhibiti Ukanda wa Gaza.

Bendera za rangi ya njano za kundi la Fatah zilitawala uwanja wa Gaza katika maandamano makubwa kabisa ya chama hicho cha Rais Mahmoud Abbas kuwahi kufanyika katika ukanda huo tokea wapiganaji wa kundi la Hamas kuwatimuwa wapiganaji hao mwezi wa Juni.

Maandamano hayo yaligeuka kuwa vurugu baada ya kusikika kwa milio ya risasi ya kile kilichoelezwa kuwa mapambano kati ya makundi hayo hasimu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com