GAZA: Israil yatangaza italipiza mashambulio ya makombora yanayotokea Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 27.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Israil yatangaza italipiza mashambulio ya makombora yanayotokea Gaza

Israil imeagiza majeshi yake kushambulia vituo vya wanamgambo wa Kipalestina kulipiza mashambulio ya makombora yanayoendelea dhidi yake kutoka ukanda wa Gaza.

Majeshi hayo yatalenga mashambulizi yake kwa wanamgmabo wanaorusha makombora aina ya Qassam kuelekea, nchini Israil kutokea Gaza.

Uumuzi huo umepitishwa baada ya mkutano ulioandaliwa na waziri mkuu, Ehud Olmert, kwa wakuu wa usalama.

Jana usiku wanamgambo wa kipalestina walirusha makombora katika mji wa Sderot, Israil kusini na kuwajeruhi vijana wawili.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com