GAZA CITY : Kombora laripuka karibu na nyumba ya Haniyeh | Habari za Ulimwengu | DW | 25.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Kombora laripuka karibu na nyumba ya Haniyeh

Ndege ya Israel imefyatuwa kombora jana usiku wa manane ambalo limeripuka karibu na nyumba ya Waziri Mkuu wa Palestina Ismael Haniyeh kwenye kambi ya wakimbizi ya Shati inayopakana na mji wa Gaza.

Maafisa wa usalama wa Palestina wamesema kombora hilo limepiga kibanda cha bati ambapo walinzi wa Haniyeh huwa wanalala lakini banda hilo lilikuwa tupu wakati huo na hakuna mtu aliejeruhiwa.

Jeshi la Israel limesema limepiga jengo linalotumiwa na Hamas katika kambi hiyo na kwamba kuwepo kwa nyumba ya Haniyeh karibu na hapo ni bahati mbaya.

Haniyeh alilikaguwa eneo hilo lakini walinzi wake walimuondowa kwa sababu ndege za Israel bado zilikuwa angani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com