GAUHATI INDIA:Kiasi watu 10 wauwawa kwenye mashambulio ya mabomu India | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAUHATI INDIA:Kiasi watu 10 wauwawa kwenye mashambulio ya mabomu India

Watu kiasi cha kumi wameuwawa katika miripuko ya mabomu kwenye kijiji cha kaskazini mashariki mwa India.Mripuko wa kwanza ulitokea kwenye soko lenye msongamano wa watu katikati ya mji wa Gauhati kwenye jimbo la Assam nchini India.

Bomu la pili liliripuliwa nje ya sehemu ya kuwekea mafuta kando ya mji huo.

Wengi wa watu waliojeruhiwa kwenye mashambulio hayo yako katika hali mbaya lakini hakuna aliyedai mara moja kuhusika na mashambulio hayo.

Jimbo hilo la Assam, ni ngome ya uasi kwa takriban miaka 30 unaongozwa na kundi linalojiita ASOM linalopigania uhuru wa kujitenga kwa eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com