1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

DeSantis kutangaza nia ya kuwania urais Marekani

Bruce Amani
24 Mei 2023

Gavana wa jimbo la Florida Ron DeSantis atatangaza Jumatano nia yake ya kugombea urais wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4Rjwa
Gouverneur Florida Ron DeSantis
Picha: Wilfredo Lee/AP/picture alliance

DeSantis anatarajiwa kuzungumza na Elon Musk katika mahojiano ya mtandao wa Twitter, ambapo atafichua mipango yake ya kuingia Ikulu ya White House.

Mmiliki wa Twitter Musk amesema itakuwa mara ya kwanza kwamba kitu kama hicho kinafanyika kwenye mtandao wa kijamii.

DeSantis mwenye umri wa miaka 44 ni mhafidhina ambaye amekuwa akiendesha vita vinavyohusu utamaduni jimboni Florida kupinga maonyesho ambayo watumbuizaji huvaa mavazi ya jinsia tofauti na kufanya maigizo.

Huenda akawa tishio kwa Donald Trump katika uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican.

Wanasiasa hao wawili walikuwa washirika wakati wa muhula wa miaka minne wa Trump katika Ikulu ya White House.

Trump alimuidhinisha wakati wa kampeini yake ya kwanza ya ugavana.