1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Demokrasia yazidi kudorora Uturuki

7 Novemba 2016

Chama kinachoelemea upande wa jamii ya wakurd cha Kurdish Peoples democratic party HDP kimesema kitasusia bunge baada ya viongozi wao kukamatwa, wakati huo kukiwa na taarifa kuwa demokrasia inashuka nchini Uturuki.

https://p.dw.com/p/2SGVP
Türkei | Verhaftung der beiden Vorsitzenden der prokurdischen Partei HDP - Archivbilder-
Picha: picture-alliance/dpa/S. Suna

Chama cha HDP kimesema siku ya jumapili kuwa kitasitisha shughuli zake  katika bunge baada ya viongozi wake na watunga sheria wengine kushikiliwa na polisi na kimesema kuwa hakitashiriki tena katika vikao vya Bunge.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa chama hicho  Ayhan Bilgen katika eneo la Diyarbakir inasema kuwa baada ya mjadiliano na kikundi cha wawakilishi wa chama hicho katika bunge pamoja na viongozi wakuu wa bodi, wamekubaliana kusitisha juhudi zake katika bungeni kufutia kila kitu ambacho kimetokea,

Msemaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa chama chao, ambacho ni chama kikuu cha pili cha upinzani hakijitoi kabisa bungeni na wawakilishi wa chama hicho wataendelea kuwa wanachama wa bunge lakini hawatashiriki  katika vikao vya bunge pamoja na vikao vya tume.

Viongozi wa HDP pamoja na watu wengine saba walikamatwa na polisi siku ya ijumaa baada ya kushindwa kuwasili kwa ajili ya kuhojiwa na waendesha mashitaka katika ya uchunguzi wa kukabiliana na ugaidi, Serikali ya Uturuki inakishutumu chama cha HDP kuwa na mafungamano na chama cha wafanyakazi cha kikurdi PKK madai ambayo hata hivyo chama hicho kinayakanusha.

Ukandamizaji dhidi ya chama cha HDP ambacho kiliandika historia mwaka jana baada ya kuwa chama cha kwanza cha Kikurd kupata zaidi ya asilimia kumi ya kura na kuingia katika bunge, umekosolewa sana na serikali za magharibi pamoja na makundi ya haki za binadamu.

Kukamatwa vya viongozi hao ni shambilio la haki ya kujieleza

Mtafiti kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la human rights watch Emma Sinclair Webb amesema katika taarifa yake wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa kitendo cha kuwashikilia wabunge ambao walichaguliwa katika misingi ya demokrasia kinachoonekana nchini Uturuki leo ni shambulio la haki ya kujieleza kisiasa  na ushiriki kwa mamilion ya wapiga kura, na ni kitendo cha kushindwa kutii kanuni za msingi kwa nchi yoyote ambayo inasema kuwa ni ya kidemocrasia na kuongozwa katika misingi ya sheria na haki za binadamu.

Türkei Kurden Protest in Ankara
Polisi wakikabiliana na waandamanaji mjini AnkaraPicha: Getty Images/AFP/A. Altan

Mwanasheria wa HDP Ercan Kanar, ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo hicho na kusema kuwa kuwashikilia viongozi waliochaguliwa na wananchi ni kudharau haki zao.

"wanapozunzumza nje au ndani ya bunge wanafikisha malalamiko ya watu, ni matakwa ya watu ambayo yanaletwa mbele ya bunge, kwa hiyo inapikuwa kinga yao inapokuwa imevunjwa ni uhuru wa watu unaokuwa umekataliwa" alisema Kanar

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wameendelea kuiokosoa Uturuki kwa kuwakandamiza wale ambao inawashuku kuwa na uhusiano na jaribio la mapinduzi la  la Julai 15 na 16 zaidi ya mahakimu 110,000, walimu , askari polisi na wafanyakazi wa Umma wamekuwa wakikamatwa na kushikiliwa, kwa upande mwingine magazeti 170, vituo vya televisheni na mshirika ya habari vimefungwa huku waandishi wa habari 2,500 wakiachwa bila kazi.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/dw English

Mhariri:Yusuf Saumu