COLOMBO.Mapigano makali yazuka kati ya jeshi la serikali na waasai wa Tamil tigers | Habari za Ulimwengu | DW | 12.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO.Mapigano makali yazuka kati ya jeshi la serikali na waasai wa Tamil tigers

Serikali ya Sri Lanka imeripoti juu ya kuzuka kwa mapigano makali kati ya majeshi yake na waasi wa Tamil Tigers na kwamba wanajeshi wake 43 wameuwawa.

Habari zinasema wanajeshi wengine 25 hadi 30 hawajulikani waliko.

Waasi wa Tamil Tigers wamesema wapiganaji wao 10 waliuwawa wakati serikali ya Sri Lanka inadai kuwauwa wapiganaji 200 wa Kitamil.

Hujuma za mizinga ziliendelea usiku wa kuamkia leo kaskazini mwa kisiwa cha Jaffna eneo linalodhibitwa na wanajeshi wa serikali, likikatwa na sehemu nyengine kwenye vituo vya waasi.

Ikiingiwa na wasiwasi kwa sababu ya kupamba moto kwa matumizi ya nguvu Marekani imezitaka pande zote mbili kusitisha uhasama kabla ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu mjini Geneva.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com