Colombo: Mapigano Sri Lanka baina ya majeshi ya serekali na waasi wa Tamil Tiger. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo: Mapigano Sri Lanka baina ya majeshi ya serekali na waasi wa Tamil Tiger.

Si chini ya waasi 15 wa chama cha Tiger cha Watamil huko Sri Lanka wameuwawa katika mapigano na majeshi ya Sri Lanka mwishoni mwa wiki. Wanajeshi wawili wanasemekana pia wameuwawa baada ya kutokea mapigano katika wilaya za Vavuniya na Muhamalai. Mapambano hayo mbali mbali ni sehemu ya hujuma zinazofanywa na jeshi la serekali katika maeneo yanayoshikiliw ana wapiganaji wa chini kwa chini katika mkoa wa Jafna, baada ya majeshi ya serekali kuwaondoa waasi kutoka mashariki ya nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com