Chissano azawadiwa tuzo ya Mo Ibrahim
22 Oktoba 2007Matangazo
Kamati hiyo ya tuzo inayoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan imeutambua mchango mkubwa wa kiongozi huyo wa zamani.
Licha ya zawadi hiyo ya dola milioni tano kwa mshindi pia kuna zawadi ya doka laki mbili kwa muda wa miaka kumi mfululizo amabzo mshindi atazitunikia miradi mbali mbali ya maendeleo nchini mwake.
Zainab Aziz alizungumza na Dr.Salim Ahmed Salim ambaye ni mmoja wa wanakamati wa taasisi ya Mo Ibrahim na kwanza anaelezea kilichozingatiwa na vigezo vilivyotumika kumteua mshindi.
Uteuzi wa rais mstaafu Chissano umepongezwa pia na wasomi mbali mbali mmoja wapo ni Profesa Mwesiga Baregu, muadhiri muandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha siasa.