1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaonya juu ya kuendelea vita dhidi ya Iran

23 Machi 2026

China imesema hali ya uchumi duniani itakuwa mbaya ikiwa vita dhidi ya Iran vitaendelea na hatari kubwa zaidi ya kuvuruga uthabiti mashariki ya kati

https://p.dw.com/p/5AuiD
Jengo la serikali mjini Tehran lilivyoharibiwa kwa mashambulio ya Marekani na Israel
Jengo la serikali mjini Tehran lilivyoharibiwa kwa mashambulio ya Marekani na IsraelPicha: Kyodo/picture alliance

China imeonya kwamba kufanyika mashambulio zaidi katika eneo la Mashariki ya kati ni hatua itakayohatarisha kutokea hali isiyoweza kudhibitiwa kwenye kanda hiyo inayokabiliwa na vita.

Tamko la China lililotolewa na wizara ya mambo ya nje kupitia msemaji wake Lin Jian, limefuatia vitisho vilivyotolewa Jumamosi na rais Donald Trump vya kutaka kuishambulia mitambo ya nishati ya Iran.

Lin Jian amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu kwamba, vita vinavyoendelea na athari zake katika mlango bahari wa Hormuz vinatishia usalama wa nishati duniani pamoja na usambazaji mafuta kwa China na hatua ya kutumiwa nguvu itasababisha hali kuwa mbaya zaidi.

China yatahadharisha kuhusu athari za mivutano kati yake na Marekani

Li Jian amesema,Beijing inaendeleza mawasiliano na pande zote kuhusu hali inayoendelea na iko tayari kusaidia kupunguza mivutano na kumaliza vita.

Kadhalika, Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati la IEA, Fatih Birol ametahadharisha kwamba uchumi wa dunia unakabiliwa na kitisho kikubwa kwasababu ya vita ya Iran na hakuna nchi itakayosalimia na athari za mgogoro huo ikiwa utaendelea katika mkondo wa sasa.