1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaaita Marekani kuwa dola la ulaghai

Sudi Mnette
30 Septemba 2023

Wizara ya mambo ya nje ya China imeiita Marekani kuwa "dola la uongo", wakati ikiijibu vikali ripoti ya Marekani, iliyoituhumu China kwa kutumia mabilioni ya fedha kila mwaka katika jitihada zake kupotosha habari.

https://p.dw.com/p/4X0Td
Südkorea | Gespräche zwischen Korea, China und Japan
Picha: Yonhap News/picture alliance

Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema China intumia uchujaji wa taarifa, udhibiti wa data pamoja na kuvinunua kwa siri vyombo vya habari vya kimataifa ili kutimiza malengo yake.Sasa katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya China imesema ripoti hiyo haijazingatia ukweli, na yenyewe kimsingi ni habari ya uwongo.Ripoti ya Marekani imetolewa katika kipindi kilichogubikwa na utata kuhusu majaribio ya China ya miaka ya hivi karibuni ya kuongeza ufuatiliaji katika vyombo vya habari vinavyosimamiwa na serikali kimataifa. Kadhalika inataka kupambana na mtazamno hasi dhidi ya taifa hilo ambao inahisi unaenezwa na vyombo vya habari ulimwenguni.