Chama cha Kansela Merkel chashindwa katika mikoa miwili | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Chama cha Kansela Merkel chashindwa katika mikoa miwili

Matokeo ya uchaguzi katika mikoa ya Ujerumani yanaonesha kuwa Chama cha Kansela Merkel cha Christian Democrat party, ,na washirika wake kimeshindwa kwa wingi wa kura katika mikoa mitatu, huku kikishinda mkoa mmoja

default

Dieter Althaus,Waziri Mkuu wa Mkoa wa Thueringen, ambaye pia alikuwa mgombea wa CDU

Katika mkoa wa magharibi mwa Ujerumani wa  Saarland  na Thuringia uliyoko katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki  chama hicho cha CDU kimepata asilimia 34.5 na 32.5 ya kura.

Muungano wa vyama vitatu vya Social Democrats SPD,kile cha mrengo wa shoto cha “Linke” pamoja na kile cha walinzi wa mazingira, unaonekana dhahiri kushinda katika mkoa wa Saarland.

Katika mkoa wa Thuringia bado haijawa wazi  iwapo chama cha  Social Democrats ambacho kimepata kura chache kuliko kile cha Linke, kimekubali kuingia katika muungano na vyama vingine kikiwa na sauti ndogo.

Stanislaw Tillich / Sachsen

Waziri Mkuu wa Saxony kupitia CDU Stanislaw Tillich, baada ya ushindi hapo jana

Katika mkoa wa mashariki wa Saxony chama cha Kansela Merkel kimepata asilimia 41 ya kura kiwango ambacho ni sawa na kile ilichopata katika uchaguzi uliyopita.Chama kinachounga mkono wafanyabishara cha Free Democrats, FDP  kimepata asilimia kumi ya kura ikiwa ni onagezeko la asilimia 4.

Waziri Mkuu wa mkoa huo wa Saxony  Stanislaw Tillich kutocha chama cha CDU Stanislaw Tillich aliwashukuru wananchi  kwa kukipa tena ushindi chama chake.

Baadhi ya wadadisi wanaona matokeo katika mikoa hiyo, ni mtihani muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani Septemba 27 mwaka huu.

Kansela Merkel anategemea kuunda muungano na chama cha  FDP, baada ya chaguzi zote hizo, ili kuweza kuweka mabadiliko katika mfumo wa kodi na sera nyinginezo.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

 • Tarehe 31.08.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/JLqJ
 • Tarehe 31.08.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/JLqJ
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com