1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cape Canaveral : Chombo kuchunguza uhai katika sayari ya Mars

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBc7

Chombo cha uchunguzi cha anga za juu cha Marekani kimeanza safari ya miezi 10 kwenye sayari ya Mars ambapo kitatafiti ishara za kuwepo kwa uhai.

Chombo hicho cha Phoenix Mars Lander kimetangana na roketi ya Delta II baada ya kufyetuliwa kutoka katika Kituo cha Anga za juu cha Kennedy kwenye mji wa Cape Canaveral katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Phoenix kinatarajiwa kutua katika sayari ya Mars hapo Mei 25 mwaka 2008 baada ya kusafiri kilomita milioni 680 za anga za juu.Wakati wa shughuli yake ya miezi mitatu mkono wa roboti wa chombo hicho utachukuwa sampuli za udongo na kuangalia ishara za kuwepo kwa uhai wakati wa zamani au hivi sasa.

Wanasayansi wengi wanaona kuwepo kwa ishara za mito ya kale na bahari katika sayari ya Mars na wanaamini kwamba sayari hiyo yumkini iliwahi kuwa na aina fulani ya uhai.