BONN: Wataalamu wajadili mabadiliko ya hali ya hewa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BONN: Wataalamu wajadili mabadiliko ya hali ya hewa

Wataalamu na wajumbe wa serikali kutoka nchi 190 wanakutana mjini Bonn,Ujerumani katika kikao kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa kuhusika na mabadiliko ya hali ya hewa.Mkutano huu wa majuma mawili unafanya matayarisho ya mkutano wa kilele utakaofanywa Bali nchini Indonesia katika mwezi wa Desemba.Wataalamu wanaopendekeza kuwa hatua za dharura zichukuliwe kupunguza ongezeko la joto duniani,wanatumaini kuwa mkataba mpya utapatikana kuchukua nafasi ya Rasimu ya Kyoto ambayo muda wake unamalizika mwaka 2012.Siku ya Jumatatu,Marekani na China-nchi zinazochafua zaidi mazingira na zilizokataa kutia saini Mkataba wa Kyoto,zilipinga mapendekezo ya Umoja wa Mataifa ya kuwasilisha ripoti za Umoja wa Mataifa katika mkutano ujao wa Bali.Ripoti mpya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Ijumaa mjini Bangkok imesema,ulimwengu una miaka minane tu yaani hadi mwaka 2015,kuanza kupunguza utoaji wa gesi chafu inayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira au sivyo uchumi duniani utakuwa na madhara makubwa mno.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com