1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Ruto kukutana mjini Washington

22 Mei 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumkaribisha leo katika ikulu ya White house mjini Washinton Rais wa Kenya William Ruto kwa ziara ya siku tatu.

https://p.dw.com/p/4g9jZ
Kenya/USA Rais wa Kenya William Ruto akiweka shada la maua kwenye makaburi ya Martin Luther King Jr na Corett Scott King
Rais wa Kenya William Ruto akiweka shada la maua kwenye makaburi ya Martin Luther King Jr na Corett Scott King nchini Marekani.Picha: John Bazemore/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Ziara hiyo inafanyika katika wakati ambao taifa hilo likijitayarisha kuwapeleka askari wake nchini Haiti kama mpango unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kujaribu kuyadhibiti magenge ya uhalifu yanayoongoza hujuma katika taifa hilo la Karibian.

Zaidi ya askari 1000 wa Kenya  wanatazamiwa kuwasili Haiti hivi karibuni kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kudhibiti magenge hayo ya uhalifu. Mataifa mengine yanayotarajiwa kuinga mkono Kenya ni  Bahamas, Barbados, Benin, Chad na Bangladesh.

Kando na suala la Haiti, Juhudi za kujenga mahusiano ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili pia zinatarajiwa kuwa ajenda ya mkutano wao.

Marekani kwa miaka mingi imekuwa ikishirikiana na Kenya katika juhudi za kupambanana ugaidi barani Afrika ikiwemo kupambana na kundi la Al Shabab.