1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bhutto azindua kampeni yake ya uchaguzi

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVU3

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto leo amewasili kaskazini-magharibi ya Pakistan kuzindua kampeni yake ya uchaguzi.Bhutto ametangaza manifesto ya kugombea uchaguzi,licha ya vyama vyingine vya upinzani kutoa mito ya kususia uchaguzi wa Januari 8.

Bhutto alishangiriwa na mamia ya wafuasi wa chama chake cha Pakistan People´s Party-(PPP) alipowasili Peshawar katika gari lisilopenyeka risasi.Benazir Bhutto aliewahi kuwa waziri mkuu kwa awamu mbili,ni mwanasiasa mashuhuri wa kwanza kuzindua kampeni ya uchaguzi baada ya Rais Pervez Musharraf kujiuzulu wadhifa wake wa mkuu wa majeshi na kuwa kiongozi wa kiraia.