BERLIN : Merkel aridhika na kazi ya serikali yake | Habari za Ulimwengu | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Merkel aridhika na kazi ya serikali yake

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema ameridhika na kazi ya serikali yake ya mseto inayoundwa na chama chake cha Christian Demokratik na chama cha Social Demokratik.

Katika mahojiano na Deutsche Welle ametowa wito wa kuachana na mabishano ya hadharani kati ya vyama hivyo na kuwataka wanasiasa katika vyama vyote viwili kujishugulisha zaidi na kazi ya kuongoza nchi.

Merkel amesema anapanga kutumia miaka miwili ijayo ya kipindi cha serikali yake madarakani kuzishajiisha kampuni zaidi za Kijerumani kushirikiana faida na wafanyakazi wao.

Pia amesema serikali yake ya mseto inapanga kuanzisha mpango wa kuwajumuisha vizuri zaidi raia wa kigeni wanaoishi nchini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com