BEIRUT: Maandamano makubwa dhidi ya serikali ya Siniora | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Maandamano makubwa dhidi ya serikali ya Siniora

Nchini Lebanon,maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu Beirut,wameitaka serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi iondoke madarakani.Makundi mengi yaliitikia mito ya chama cha Kishia cha Hezbollah chenye siasa kali,na washirika wake wanaoiunga mkono Syria.Lakini hata kiongozi wa upinzani Michel Aoun alie Mkristo,amemtaka Siniora ajiuzulu na ametoa mwito wa kuunda serikali mpya ya umoja.Wafanya maandamano waliziba barabara na wakapiga mahema karibu na ofisi za serikali.Idadi kubwa ya vikosi vya usalama vilitawanywa katika mji wa Beirut.Waziri mkuu Siniora amesema serikali yake itabakia,licha ya kwamba hivi karibuni,mawaziri sita walioasi,walijitoa serikalini.Kwa upande mwingine,waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na waziri mwenzake wa Uingereza Bibi Margaret Beckett wamepanga kukutana na waziri mkuu Siniora.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com