BEIJING:Tarehe maalum kwa Korea Kaskazini kufunga mitambo ya nuklia haijafikiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING:Tarehe maalum kwa Korea Kaskazini kufunga mitambo ya nuklia haijafikiwa

Siku ya tatu ya mazungumzo juu ya vinu vya nuklia vya Korea Kaskazini, yamemalizika bila ya kuwekwa tarehe maalum kwa nchi hiyo kufunga vinu vyake.

Ilitarajiwa ya kwamba mazungumzo hayo yangetoa mwongozo wa kitaalam juu ya hatua zaidi za kufunga vinu hivyo.

Katika mazungumzo ya pande sita mjini Beijing, mwakilishi wa Marekani kwenye mazungumzo hayo Christopher Hill alisema kuwa anaamini kuwa Korea Kaskazini itaweza kukamilisha awamu ya pili ya ufungaji wa vinu vyake itakapofika mwisho wa mwaka huu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com