1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAVARIA:Ulaya yakumbwa na hali mbaya ya hewa

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg5

Mvua kali , hali mbaya ya hewa na mafuriko vimelikumba eneo la kati na magharibi mwa Ulaya, ambapo hapa ujerumani mtu mmoja amekufa na wengine kumi kujeruhiwa.

Mkoa wa kusini wa Bavaria umetangaza hali ya hatari ambapo baadhi ya maeneo yamefunikiwa na maji kwa urefu wa mita moja.

Uingereza ndiyo iliyoathirika zaidi na mafuriko kwa mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja, ambapo mamia ya watu wamelazimika kuokolewa