BAGHDAD: Watu takriban 60 wauwawa katika mashambulio ya mabomu | Habari za Ulimwengu | DW | 19.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu takriban 60 wauwawa katika mashambulio ya mabomu

Watu takriban 60 waliuwawa jana kufuatia mashambulio matatu ya mabomu mjini Baghdad nchini Irak. Mabomu hayo yaliripuka katika maeneo ya Washia mjini humo, huku mawili yakiliharibu soko kubwa katika wilaya ya New Baghdad.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha alikivamia kituo cha upekuzi kilichowekwa na polisi wa Irak mjini Sadr na kujiripua.

Mashambulio hayo ya jana Jumapili mjini Baghdad, ndiyo mabaya zaidi kuwahi kufanywa tangu operesheni ya kuwachakaza wapiganaji wa Irak ilipoanzishwa na jeshi la Marekani na vikosi vya Irak mnamo Jumatano wiki iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com