BAGHDAD : Mripuko wauwa watano na kujeruhi zaidi ya 100
20 Februari 2007Matangazo
Takriban watu watano wameuwawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa wakiwemo wanawake wengi na watoto baada ya bomu kuripuka kwenye gari lililokuwa na gesi aina ya chlorine kaskazini mwa Baghdad leo hii.
Gari hilo lililokuwa na bomu limeripuka karibu na mkahawa katika kituo cha mapumziko kwenye barabara kuu ya Taji kilomita 20 kaskazani mwa mji wa mkuu wa Baghdad.Gesi ya chlorine ambayo ni sumu inaweza kusumbuwa mfumo wa kupuwa na hutumika kwa ajili ya kusafishia maji.
Bomu jengine lililotegwa kwenye gari pia limeripuka mjini Baghdad karibu na kituo cha mafuta katika wilaya ya Sadiya na kuuwa watu watano na kujeruhi wengine 11.