1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Majeshi ya Marekani yasitisha mashambulizi yake.

9 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CETf

Majeshi ya Marekani nchini Iraq yamekamilisha mashambulizi yake yaliyochukua muda wa siku sita katika eneo la magharibi ya jimbo linalokaliwa na Wasunni wengi la Al Anbar.

Msemaji wa jeshi la Marekani limedai kuwa zaidi ya magaidi wa Al Qaida 50 wameuwawa katika msako huo.

Wanajeshi wawili wa Marekani pia wameuwawa katika mapigano hayo. Mashambulizi hayo ya kijeshi yamekuja muda mfupi tu kabla ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Iraq.

Kura hiyo ya maoni kuhusiana na katiba hiyo itasafisha njia kwa ajili ya uchaguzi mkuu hapo Desemba mwaka huu.

Wakati huo huo , serikali ya Iraq imetangaza hatua kadha za usalama , ikiwa ni pamoja na hatua za kuzuwia watu kusafiri ovyo na kupiga marufuku silaha, kwa muda wa siku kadha kabla na baada ya kura ya maoni hapo Oktoba 15.