Baghdad. Mabomu yaua watu 20, na miili 39 yaokotwa ikiwa na majeraha ya risasi. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Mabomu yaua watu 20, na miili 39 yaokotwa ikiwa na majeraha ya risasi.

Kiasi watu 20 wameuwawa katika mashambulio kadha nchini Iraq, ikiwa ni pamoja na watu watano ambao wamefariki kutoka na shambulio la kujitoa mhanga katika gari nje ya eneo la ibada katika mji mtakatifu wa Washia wa Karbala.

Polisi pia walipata miili ya watu 39 ambayo ilikuwa na alama za risasi mjini Baghdad ambao wanaonekana kuwa walikuwa wahanga wa mauaji ya kulipiza kisasi baina ya Waarabu wa madhehebu ya Sunni na Washia.

Kwingineko nchini Iraq, jeshi la Marekani limetangaza kuwa wanajeshi wawili wa jeshi hilo la Marekani wameuwawa katika mapigano yaliyotokea katika jimbo la Anbar, na kufikisha idadi wanajeshi wa Marekani ambao wameuwawa nchini Iraq mwezi huu kufikia 42.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com