1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock afanya ziara ya tano nchini Israel

Zainab Aziz
14 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa kuwasili nchini Israel kwa ziara ya tano tangu Israel iliposhambuliwa na wapiganaji wa Hamas mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4cO6b
Berlin, Ujerumani | Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Baerbock atakutana na waziri mwenzake wa Israel pamoja na waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Jair Lapid.

Baerbock na wenyeji wake wanatazamiwa kuzungumzia juu ya mashambulio ya ardhini ambayo Israel inapanga kufanya kwenye mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza na pia juu ya hali ya Gaza kwa jumla.

Soma pia:Wasiwasi wa kimataifa waongezeka kufuatia operesheni ya Israel Rafah

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, ameitaka Israel itenge uchochoro wa usalama kwa ajili ya Wapalestina walio katika mji wa Rafah.