AWJA: Waombolezaji wa kifo cha Saddam waapa kulipiza kisasi | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AWJA: Waombolezaji wa kifo cha Saddam waapa kulipiza kisasi

Mamia ya waombolezaji walikusanyika katika kaburi la rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein kwa maombi. Wameapa kulipiza kisasi kufuatia kunyongwa kwa kiongozi huyo.

Saddam alizikwa katika kijiji alikozaliwa cha Awja karibu na mji wa Tikrit kaskazini mwa Irak. Wana wa kiume wa Saddam Uday na Qusay waliouwawa na wanajeshi wa Marekani mnamo mwaka wa 2003 walizikwa kijijini humo kwenye kiwanja cha familia yao.

Wakati huo huo, wapalestina zaidi ya 1,000 walifanya maandamano katika barabara za mji wa Jenin huko ukingo wa magharibi wa mto Jordan wakilaani kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com